News And Other Stuff.

KLABU YA ASANTE KOTOKO YA GHANA YAPATA AJALI MBAYA.


Basi la timu ya Asante Kotoko lililopata ajali likiwa limeharibika.

Taarifa kutoka Ghana zinasema kwamba pametokea ajali ya gari lililokuwa limebeba miongoni mwa timu kongwe nchini humo Asante Kotoko.

Mlezi wa timu hiyo ni mfalme wa Ashanti.

Timu hiyo ilikuwa inarejea katika mji wake ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini humo , Kumasi baada ya mchezo wa ligi kuu mjini Accra dhidi ya Inter Allies FC.

Ajali hiyo imetokea katika sehemu iitwayo Nkawkaw kilomita 150 kutoka mji mkuu wa Ghana, Accra.

Inasemekana kuwa baadhi ya wachezaji wameumia vibaya akiwemo pia kocha wa timu hiyo na pia kuna kifo cha mtu mmoja.

Kikosi cha timu ya Asante Kotoko kilichopata ajali.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.