CHELSEA YAPATA KOCHA MPYA

Antonio Conte kwa sasa kocha wa Chelsea
Meneja wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte ameteuliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Chelsea ya Uingereza. , kuanzia mwishoni wa msimu huu.
Mkufunzi huyo wa zamani wa Juventus mwenye umri wa miaka 46 ataanza kutumikia mkataba wake wa miaka mitatu baada ya kuongoza Italia michuano ya Euro 2016.
Conte atakuwa Mwitaliano wa tano kuwa meneja wa Chelsea baada ya Gianluca Vialli, Claudio Ranieri, Carlo Ancelotti na Roberto di Matteo.
Antonio Conte

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.