PAUL POGBA KUCHEZA NA SOUTHAMPTON.
Kiungo aliyeigharimu Man Utd kiasi cha Pauni milioni 89, Paul Pogba amejinasibu kuwa tayari kuanza kuitumikia klabu hiyo katika mchezo ambao utawakutanisha dhidi ya Southampton.
Pogba ambaye hakuwa sehemu ya kikosi kilichofanya vyema katika mpambano wa ufunguzi wa ligi mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Bournemouth na kupata ushindi wa mabao matatu kwa moja, amesisitiza kuwa tayari kucheza alipohojiwa na kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini England.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, amesema tayari ameshafanya mazoezi ya kutosha tangu alipowasili klabuni hapo majuma mawili yaliyopita na ameona yupo fit kuwakabiliwa Southampton, ambao watafunga safari ya kuelekea Old Trafford hapo kesho.
Hata hivyo amedai kwamba, maamuzi ya meneja Jose Mourinho ndio yatakayotoa nafasi kwake kucheza ama kuendelea kukaa nje, hivyo anasubiri suala hilo japo anajihisi yupo tayari kwa mapambano.
Mshabiki wengi wa soka duniani wanasubiriki kumuona Pogba akicheza tena katika kikosi cha Man Utd, baada ya kuondoka klabuni hapo mwaka 2012 kwa kigezo cha kukosa nafasi katika utawala wa babu Ferguson, na ujio wake kwa kipindi hiki ulikua gumzo kutokana na ada ya usajili iliyotumika kumrejesha katika himaya ya mashetani wekundu.

Leave a Comment