MANCHESTER CITY WAONDOSHWA NJE NA MONACO.

Manchester City imeondolewa katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya kwa magoli ya ugenini katika mechi dhidi ya Monaco.
 Mechi hiyo ilimalizika kwa magoli 3-1 lakini kwa jumla ya mabao 6-6.
Monaco na Manchester City walionesha mchezo wa kuvutia na kusisimua, wakianza mchezo wa duru ya pili Man City wakiwa mbele kwa mabao 5-3.
Kipindi cha kwanza, kiliongozwa na Monaco. Fabinho, Tiemue Bakayoko na Bernardo Silva walitawala eneo la kiungo, huku Kylian Mbappe akitishia ngome ya City kila wakati.Monaco
Na ni Mbappe ambaye baba yake ana asili ya Cameroon ndio aliandika bao la kwanza katika dakika ya saba baada ya kuunganisha krosi ya Silva.
City hawakuweza kujibu mapigo na katika dakika ya 27, Monaco walijikita mbele kwa kuandika bao la pili.
Goli kwa mara nyingine tena lilitokea upande wa kushoto, Thomas Lemar akilisha mpira mtamu kwenda kwa Benjamin Mendy ambaye alichonga krosi iliyopachikwa kimyani na Fabinho.
Baada ya mapumziko City walionekana kubadilika, wakitumia mabeki wao kupanda. Lakini walipoteza nafasi kadhaa, Sergio Aguero akipoteza nafasi nyingi, kabla ya Leroy Sane kufunga goli katika dakika ya 71.
Mchezo ulimalizika kwa mabao 3-1.
VIKOSI VYA TIMU ZOTE MBILI VILIKUWA HIVI.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.