Nay wa Mitego Amkaushia Rais Magufuli Pamoja na Kuachiliwa Huru kwa Amri Yake.
Rapa huyo alishikiliwa na jeshi hilo kwa siku mbili baada ya wimbo wake mpya ‘Wapo’ kuonekana hauna maadili.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya kutoka kituo cha polisi alipokuwa ameshikiliwa, Nay ameishukuru serikali pamoja na wadau mbalimbali ambao walikuwa wanampambania.
“Nawashukuru sana watu wa media, wanasheria wangu ndugu jamaa na marafiki kwa upendo waliouonyesha kwangu. Pia naishukuru serikali kwa hichi walichokifanya, sasa hivi sina kubwa la kuongea wimbo umeruhusiwa nashukuru na nimefurahi kusikia hivyo,” alisema Nay wa Mitego.
Rapa huyo amesema kwa sasa anajipanga kufanya maandalizi ya kuandaa video kwajili ya wimbo huo.
Katika taarifa iliyotolewa mapema leo na Rais Magufuli alisema wimbo huo ni mzuri lakini aongezee changamoto nyingine zilizopo kwenye jamii.
Leave a Comment