Mwanafunzi Udom Akutwa na Misokoto 826 ya Bangi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake leo asubuhi, kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema kuwa mwanafunzi huyo alikamatwa Mei 9 mwaka huu kufuatia msako mkali uliofanywa na jeshi hilo chuoni hapo ambapo mtuhumiwa alikutwa na jumla ya misokoto 826 ya bangi yenye uzito wa kilo 2.8 akiwa ameiweka kwenye mifuko ya nailoni chumbani kwake.
Mambosasa amesema kuwa mtuhumiwa alipohojiwa alisema kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo ya kuuza bangi kwa kipindi cha miaka minne tangu alipojiunga na chuo hicho na kwamba alikuwa akiwauzia wanafunzi wenzake.
Leave a Comment