EVERTON NA GOR MAHIA MATOKEO HAYA HAPA.




Mchezo wa kirafiki kati ya Everton ya nchini Uingereza dhidi ya Gor Mahia ya nchini Kenya umemalizika jioni hii kwa vijana hao wa Ronald Koeman kuibuka na ushindi wa 2-1.




Mchezo huo ulianza taratibu na kadri muda ulivyokuwa ukienda mchezo huo uliongezeka kasi zaidi huku Everton wakionekana kucheza kwa umakini mkubwa.



Mshambuliaji mpya wa klabu hiyo aliyetokea Manchester United, Wayne Rooney aliianza kuifungia bao la kwanza ambalo halikudumu kwa dakika chache baada ya Gor Mahia kusawazisha na kuufanya mchezo huo kipindi cha kwanza kumalizika kwa 1-1.



Katika kipindi cha pili Everton walikuja kwa kasi zaidi hali ambayo iliwafanya Gor Mahia kucheza kwa makini zaidi hatua ambayo haikuzaa matunda.
Dakika ya 78 za mchezo, Everton waliweza kumiliki mchezo zaidi ya kufanikiwa kupata goli la pili na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa 2-1.


Raism mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete(wa pili) alikuwepo uwanja wa Taifa akishudia mechi.

shabiki aliyemvamia Rooney katikati ya mchezo.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.