HALIMA MDEE AACHILIWA KWA DHAMANA YA TSH MIL 10.

Image may contain: 1 person, glasses
Mhe. Halima Mdee ameachiwa kwa dhamana ya Shilingi Milioni 10 pamoja na wadhamini wawili baada ya kusomewa shitaka moja la kutoa lugha ya matusi.

Mbunge huyo wa Kawe alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu hivi leo baada ya kukamatwa na jeshi la polisi wiki iliyopita,ambapo atarudi tena Mahakamani hapo 7 mwezi wa 8 mwaka huu.

Ikumbukwe kuwa Mbunge huyo alikamatwa na polisi kwa madai ya kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli wakati alipokutana na waandishi wa habari wiki iliyopita.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.