ZITTO NA HASHIM RUNGWE WAKUTANA KUJADILI UCHAGUZI


Nimekutana na Mwenyekiti wa CHAUMMA, ndugu Hashim Rungwe Spunda katika mwendelezo wa kukutana na Viongozi wa Juu wa Vyama vya Upinzani nchini. Nafurahi tumekuwa na mazungumzo mazuri sana, ndugu Rungwe ni mzee mwenye busara na hekima nyingi sana. 


Ni matarajio yetu kuwa mazungumzo haya yatazalisha jambo zuri kwa Taifa.

Mazungumzo haya ni sehemu ya maelekezo niliyopewa na Kamati Kuu ya ACT Wazalendo kuwafikia wadau wote wa Demokrasia nchini ili kuweka mikakati ya pamoja ya hatua za ziada za kuchukua ili kuboresha mazingira ya chaguzi huru na za haki nchini.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Disemba 21, 2017
Dar es Salaam



No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.