Askofu Gwajima Apiga Marufuku Watu Kulia Kwenye Msiba Wa Mama Yake


Mama Mzazi Wa Askofu Wa Kanisa La Ufufuo Na Uzima, Josephat Gwajima, Bi. Ruth Paulo Gwajima Ameagwa Na Kuzikwa siku ya jana Salasala Jijini Dar, Ambapo Msiba Wake Umeacha Historia Kwa Kuhudhuriwa Na Umati Mkubwa Ikiwa Ni Pamoja Na Waombolezaji Kuzuiwa Kulia Kwa Kile Kilichoitwa “Shujaa Amerudi Nyumbani…”



Akizungumza Kwenye Msuba Huo Askofu Gwajima Alisema “Hata Utakapoanza Kulia Unashangaza Tu, Mama Ameondoka Yuko Mbinguni, Anaangalia, Kwahiyo Jipe Moyo Mkuu Na Jue Tafasiri Halisi Ya Kifo Ni Nini. Tafasiri Halisi Ya Kifo Ni Kuhama Kutoka Mji Mwingine Kwenda Mji Mwingine. Ulikuwa Unakaa Kigilagila Geti Rumo, Sasa Umehamia Madale. Ni Wewe Yuleyule. Ulikuwa Unakaa Mbonyokwa Sasa Uko Manzese Kwa Tumbo. Ulikuwa Unakaa Manzese Uwanja Wa Fisi Sasa Unahamia Manzese Kwa Bonge, Ni Wewe Huyohuyo. Mama Alikuwa Anakaa Duniani Amehamia Mbinguni Lakini Ni Yeye Yuleyule Hajapotea. Na Wale Wanaodumu Katika Imani Watamuona Tena. Kwahiyo There Is Nothing, Hakuna Haja Ya Kulia, Hakuna Haja Ya Kuomboleza, Ila Tu Kunakuwa Na Family Entiesment Kutokujua Tafasiri Ya Kifo Kunasumbua Sana Kwa Wakristo. Tujifunze Kuwakubali Watu Wakiwa Hai. Mtu Akifanya Vizuri Mwambieni Well Done, Kwa Sababu Pongezi Zozote Anazopewa Mtu Aliyekufa Hapewi Yeye.”


A post shared by Bishop Josephat Gwajima PhD 🌍 (@bishopgwajima) on



Pia Msiba Huo Ulihudhuriwa Na Viongozi Mbalimbali Wa Serikali Akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Mbunge Wa Vunjo James Mbatia, Mbunge Wa Arusha Mjini Godbless Lema Na Bernard Membe.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.