Odinga atarajiwa kuapishwa leo na upinzani Kenya



Hali ya wasiwasi imetanda nchini Kenya baada ya kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo Bwana Raila Odinga, kushikilia kuwa ataapishwa leo kama rais wa nchi hiyo.
PolisiPolisi

Muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) umesema hafla hiyo itafanyika katika uwanja wa Uhuru Park, Nairobi.

Baada ya sherehe hizo kuahirishwa mwezi uliopita, muungano mkuu wa upinzani nchini humo-NASA, bado unaendelea na msimamo wake wa kuwaapisha viongozi wake Raila Odinga na Stephen Kalonzo Musyoka, kama Rais na Makamu wa rais wa Jamhuri ya Kenya.

Maafisa wa polisi walifika asubuhi na mapema katika uwanja wa Uhuru Park, Nairobi unaopanga kutumiwa na muungano wa Nasa kwa shughuli ya kumuapisha Bw Odinga.

Kituo cha habari cha kibinafsi cha Citizen kimeripoti kuwa maafisa wa polisi wameamrishwa kuondoka katika uwanja wa Uhuru Park.

Wafuasi wa upinzani waliokuwa wanasafiri kuelekea Nairobi ambao walizuiliwa awali mjini Voi wameachiliwa na kuruhusiwa kuendelea na safari

Mji wa Voi unapatikana takriban kilomita 330 mashariki mwa mji huo mkuu wa Kenya.

Afisa wa polisi amewaambia wanahabari kwamba madereva wa mabasi hayo walikuwa wamevunja sheria kadha za barabarani.

Wafuasi wa upinzani nchini Kenya wameanza kuingia uwanja wa Uhuru Park baada ya polisi kuondoka.

Baadhi wanazunguka uwanja huo wakiimba 'Uhuru Must Go.

Raila Odinga anadai alishinda uchaguzi urais wa tarehe 8 Agosti 2017

Mahakama ya Juu ilibatilisha matokeo ya uchaguzi huo wa Agosti na kuagiza uchaguzi urudiwe, lakini Bw Odinga akasusia

Odinga amesema hatambui ushindi wa Bw Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa marudio wa 26 Oktoba

Serikali imeonya kuwa hatua ya kuapishwa kwa Bw Odinga ni uhaini wa kiwango cha juu.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.