Rais Magufuli afanya mabadiliko wizara ya madini, Amteua Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri
Mhe. Doto Mashaka Biteko ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe na alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya muda iliyochunguza madini ya Tanzanite.
Kufuatia uteuzi huu Wizara ya Madini sasa itakuwa na Waziri na Naibu Mawaziri wawili.
Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi huu kwa lengo la kuongeza nguvu kutokana na uwingi wa majukumu katika Wizara ya Madini.
Mhe. Doto Mashaka Biteko ataapishwa Jumatatu tarehe 08 Januari, 2018 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Januari, 2018

Leave a Comment