Matokeo Ya Kidato Cha Nne 2018 Yatangazwa, Bonyeza Hapa Kutazama.
Katika matokeo hayo mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi ni kutoka shule ya sekondari Ilboru ya Arusha, anaitwa Hope Mwaibanje.
Hata hivyo Necta imesema kiwango cha ufaulu katika matokeo ya kidato cha nne, kimeongezeka kwa asilimia 1.29, kutoka asilimia 77.09 mwaka 2017 hadi asilimia 78.38 mwaka 2018.
Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk. Charles Msonde |
Amesema watahiniwa tisa wasichana kati ya 10 bora kitaifa, katika matokeo haya ni kutoka Shule ya Wasichana ya Mtakatifu Francis ya Mbeya, huku msichana wa 10 bora kitaifa, anatoka shule ya Wasichana ya Anwarite ya Kilimanjaro.
Katika matokeo hayo, watahiniwa 252 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu na kati yao, 71 ni wa kujitegemea huku wawili kati yao wakiandika matusi.
Leave a Comment