CLABU YA VALENCIA YAMFUKUZA KAZI KOCHA GARY NEVILLE
![]() |
| Gary Neville. |
![]() |
| Gary Neville. |
Beki wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Gary Neville amefutwa kazi na klabu ya Valencia ya Uhispania baada ya kuhudumu kama meneja wao kwa chini ya miezi minne.
Valencia walishinda mechi tatu pekee kati ya 16 walizocheza ligini chini ya Neville, na mechi 10 kati ya 28 kwa jumla katika mashindano yote.
Neville amesema alitaka kuendelea kuifundisha Valencia lakini matokeo hayakufikia viwango vinavyohitajika na klabu hiyo.
Neville alitakiwa ajiuzulu baada ya klabu hiyo kucharazwa 7-0 na Barcelona mechi ya kwanza ya nusu Copa del Rey mwezi Februari.
![]() |
| Gary Neville siku aliyosaini kuifunisha Valencia miezi nane iliyopita. |
CHANZO CHA HABARI BBC SWAHIL



Leave a Comment