Zinedine Zidane: Sioni Real Madrid bila Cristiano Ronaldo.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 yuko katika kandarasi hadi 2021 na alishinda taji lake la tano la Ballon d'Or mwezi uliopita

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane anaamini kwamba mshambuliaji nyota Cristiano Ronaldo atasalia katika klabu hiyo na haoni sababu za yeye kuondoka katika klabu hiyo ya Uhispania.

Mshambuliaji huyo wa Ureno amefunga magoli tisa katika mechi sita za vilabu bingwa lakini amefunga bao nne katika mechi 14 za la Liga msimu huu.

Kulingana na ripoti , Ronaldo amekuwa na mgogoro wa kandarasi na klabu hiyo na amehusishwa na uhamisho wa kurudi Manchester United.

Lakini Zidane alisema: Mimi hupendelea kusema kitu hicho hicho kwamba sioni Real Madrid bila Cristiano Ronaldo.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 yuko katika kandarasi hadi 2021 na alishinda taji lake la tano la Ballon d'Or mwezi uliopita
Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 yuko katika kandarasi hadi 2021 na alishinda taji lake la tano la Ballon d'Or mwezi uliopita, mbali na kufunga bao la pekee katika mechi ya fainali ya klabu bingwa duniani dhidi ya Gremio.

Licha ya kuonyesha mchezo mzuri katika mechi za vilabu bingwa, wako katika nafasi ya nne katika ligi ya La liga baada ya kushindwa nyumbani na Vilareal siku ya Jumamosi.

Cristiano Ronaldo alishindwa kufunga dhidi ya klabu ya Villareal uwanjani Bernabeu

Tangu kujiunga na Real Madrid kutoka Man United ambapo alivunja rekodi ya £80m 2009, Ronaldo ameifungia timu yake mabao 422 katika mechi 418, lakini ameshindwa kufunga katika mechi tatu za ligi.


Zidane alisema: Tunajua kilichojadiliwa , lakini kile Cristiano anachofaa kufanya ni kufikiria kucheza kama kawaida.

'Ningependa kuzungumza kuhusu mchezo wake kwa sasa na kile anachoweza kuchangia katika timu akiwa uwanjani''.

''Cristiano ni mmoja wa klabu hii, ambapo yupo. Klabu, mashabiki na kila mtu anampenda. Upande wake wa mchezo ndio nilio na hamu nao. Sitaki kuzungumzia kandarasi yake na vitu kama hivyo''.

Baada ya kushinda mechi mbili kati ya saba za ligi, Real wako na pointi 19 nyuma ya viongozi Barcelona wakiwa na mechi ambayo hawajacheza.

Alipoulizwa kuhusu hatma yake ya siku za usoni , Zidane alisema: Sifikirii kuhusu hilo.Nafanya kazi kulingana na siku ilivyo na siwezi kubadilisha hilo.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.