FAHAMU JINSI YA KUJIKINGA DHIDI YA RADI

Lightning
Radi
Radi ni nini?

Radi hutokana na kuachiliwa kwa umeme tuli, tukio ambalo hutokea kutokana na tofauti ya nguvu za umeme kati ya mawingu na ardhi.

Huwa ni cheche kubwa ya umeme kutoka angani, ambayo huwa na nguvu sana. Inaweza kusababisha moyo wa binadamu kuzima na kuacha kupiga na pia kuunguza viungo muhimu mwilini.

Zaidi ya robo tatu ya wanaonusurika baada ya kupigwa na radi hupata ulemavu wa aina fulani ambao hudumu maishani.

Radi hutoka wapi?

Mara nyingi radi hutokea kwenye sehemu ya chini ya anga, ambayo kwa Kiingereza hufahamika kama 'troposphere'.

Huwa inaenea kutoka kwa wingu moja hadi jingine au kutoka kwa wingu hadi ardhini.

Radi inaweza pia kupatikana katika mawingu ya majivu kutoka kwa volkano.
Wanaume hupigwa zaidi ya wanawake

Kwa mujibu wa Taasisi ya Serikali ya Kuzuia Ajali UIngereza (Rospa), wanaume wana uwezekano mara nne zaidi ya wanawake wa kupiwa na radi.

Hili inadhaniwa hutokana zaidi na aina ya shughuli ambazo wanaume hujihusisha nazo, ambapo uwezekano wao wa kuwa nje wakati wa mvua huwa juu mno.

Two photos of men with lightning injuries that look like flower or tree branches
Mtu aliyepigwa na radi
Wachezaji gofu mara nyingi huwa kwenye hatari zaidi kwani ndio walio na uwezekano mkubwa wa kuwa maeneo ya wazi mbali na nyumba au eneo la kujikinga mvua.

Aina tatu za kupigwa na radi

Huwa kuna aina tatu za radi ambazo zinaweza kumpiga mtu.

Moja ni kupigwa moja kwa moja, ambapo radi hukupiga na nguvu za umeme kupitia ndani ya mwili wako hadi ardhini.

Pili ni kupigwa pembeni, ambapo huwa kitu kilichokaribu nawe kimepigwa na radi, nguvu zikaruka na kukufikia.

Tatu
ni radi inapopiga ardhini na kisha kukufikia.

Utawezaje kujikinga?

  • Tafuta hifadhi pahali ambapo kuna jumbwa kubwa au ndani ya gari. Kukiwa na jumba ambalo lina kifaa cha kukinga dhidi ya radi, utakuwa salama zaidi.
  • Usiwe katika maeneo ya wazi, au kwenye mlima ulio wazi.
  • Iwapo utakosa pahala pa kujikinga mvua, punguza uwezekano wako wa kupigwa kwa kujikunyata na kujifanya mdogo zaidi. Unaweza kuchutama, kuweka mikono yako kwenye magoti na kufichwa kichwa chako ndani.
  • Usijikinge mvua chini ya miti.
  • Iwapo upo pahala ambapo kuna maji, ondoka na kukwepa maeneo ya ufukweni yaliyo wazi.
  • Utafiti umeonesha kwamba kuwa karibu na maji huongeza hatari ya mtu kupigwa na radi.
  • Kwa kuwa radi huwa nguvu za umeme, unafaa kujiepusha na vitu vya chuma vyenye ncha kali ukiwa kwenye mvua.

Kumbuka, hatari ya kupigwa na radi inaweza kuwepo kwa muda hata baada ya mvua kubwa kuacha kunyesha.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.