Picha za Nusu Utupu za Gigy Money, Sanchoka na Amber Lulu Zawapeleka Polisi .

Sekeseke la picha na video za utupu zinazopachikwa na baadhi ya warembo kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram kwa lengo la kujipatia wanaume yaani kujiuza mitandaoni (Cyber Prostitution), linadaiwa kusababisha baadhi yao kuitwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi ‘Sentro’ jijini Dar es Salaam.

Warembo hao wanahitajika kwenye Kitengo cha Kupambana na Uhalifu wa Mtandaoni (Cyber Crimes) kilicho chini ya Jeshi la Polisi Tanzania kufuatia video na picha zao za utupu kuendelea kusambaa  mitandaoni na kumomonyoa maadili ya watoto wa Kitanzania. 

Polisi wanasema kabla ya sheria kuchukua mkondo wake itabidi wawabane ili kueleza lengo lao ni nini? Kama itabainika wanajua lakini wanafanya makusudi, sheria itachukua mkondo wake na adhabu kali itawahusu.

“Wanaoitwa Sentro wapo wengi lakini kuna huyu Sanchoka (Jane Ramoy), Gigy Money (Gift Stanford) na Amber Lulu (Lulu Auggen). Hawa watoto ni shida hivyo inabidi kuwapunguza spidi na wawe mfano kwa wengine"

Ambacho watu hawakijui ni kwamba polisi hawawezi kumkamata bila kupokea malalamiko kuwa anafanya hiki na hiki mtandaoni na kisheria siyo sahihi. “Lakini kwa hawa malalamiko yapo kila kukicha,” kilinyetisha chanzo chetu.

Akizungumza na Wikienda juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) juu ya watu kama hao, Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy anafafanua kuwa, mamlaka hiyo haina mamlaka ya kumkamata mtu isipokuwa malalamiko yanapaswa kupelekwa polisi.

Kamanda Mwangasa aliliambia Wikienda kuwa, baada ya kupokea malalamiko hayo, jopo lake la wachunguzi limekuwa likizipitia ‘accounts’ zote za warembo hao ili kuwachukulia hatua stahiki haraka iwezekanavyo.

GIGY, AMBER WAJITETEA Wikienda liliwatafuta mamodo hao kwa nyakati tofuati ambapo Sanchoka hakuweza kupatikana huku Gigy na Amber Lulu wakijitetea kuwa watajieleza kwamba huwa wanafanya kwa ajili ya matangazo ya nguo.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.