Ndikumana Mume wa Irene Uwoya Afariki Dunia

Aliyekuwa mume wa muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya, mchezaji Hamad Ndikumana (39) kutoka nchini Rwanda amefariki usiku wa kuamkia leo.
Ndikumana Hamad 'Katauti' alifariki dunia ghafla katika hospitali ya mjini Kigali.Ndikumana alikuwa kocha msaidizi katika timu yake ya zamani ya Rayon Sports.
Msemaji wa timu hiyo Olivier Gakwaya ameiambia BBC kuwa Katauti jana aliendesha mazoezi kama kawaida kabla ya kurejea kwake mtaa wa Nyamirambo."Baadaye hakujihisi vizuri akaenda kununua dawa katika duka la madawa lakini lakini hali yake imeendelea kuwa mbaya ndipo amepelekwa hospitali ya CHUK alikofariki," amesema Oliver Gakwaya.

Ndikumana alichezea timu ya Rayon Sports na timu ya taifa ya Rwanda kwanzia mwaka 1998 na kuwa nahodha wa muda mrefu wa Amavubi.
Pia alicheza soka la kulipwa ulaya katika timu za Gent na Anderlecht za Ubelgiji, Omonia Nicosia na Limassol za Cyprus.
Pia alicheza soka la kulipwa ulaya katika timu za Gent na Anderlecht za Ubelgiji, Omonia Nicosia na Limassol za Cyprus.

Mwaka 2009 alifunga ndoa na nyota wa filamu ya Tanzania Irene Uwoya maarufu Oprah kabla ya ndoa yao kuvunjika rasmi miaka 3 iliyopita.
Mpaka anakutwa na umauti alikuwa akicheza katika timu ya APOP Kinyras Peyias FC ya Cyprus. Alizaliwa Oktoba 5, 1978 na mpaka anafariki dunia alikuwa ametengana na Uwoya kwa miaka mingi na alikuwa ndiye mkewe waliyefunga naye ndoa katika Kanisa Katoliki na walibahatika kupata mtoto mmoja ambaye jina lake ni Krish.

Leave a Comment