Meli ya 'Titanic II' kuzinduliwa mwaka 2018

Meli ya Titanic II yenye muundo na ukubwa sawa na ule wa meli maarufu ya Titanic iliyozama mwaka 1912 itazinduliwa na kutumika baharini kwa mara ya kwanza mwaka 2018.

Uzinduzi wa meli ya Titanic II hapo awali ulipangwa kufanyika mwaka 2016 lakini baadaye kubadilishwa na kupangwa kufanyika mwaka 2018.
Taarifa hiyo ilitolewa na msemaji na pia bilionea wa Australia Clive Palmer, ambaye pia ni mmliki wa kampuni ya kutengeneza meli.
Kampuni ya meli ya Blue Star Line imetengeneza meli ya Titanic ambayo imefanana na ile ya awali iliyozama baada ya kugonga barafu mwaka 1912.
Titanic II katika safari yake ya kwanza baharini itatoka Jiangsu, China kuelekea Dubai.
Aidha itabeba abiria 2,400 na wafanyikazi 900 huku ikiwa na vyumba 840.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.