MWANAJESHI WA MAREKANI ALIYEASI NA KUHAMIA KOREA KASKAZINI AFARIKI DUNIA.
![]() |
James Dresnok mwanejeshi wa mwisho wa Marekani aliyeasi na kuhamia kuishi nchini Korea Kaskanizi. |
James Dresnok mwanejeshi wa mwisho wa Marekani aliyeasi na kuhamia kuishi nchini Korea Kaskanizi, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 74 mwaka uliopita, kwa mjibu wa watoto wake.
Watoto wake Bw. Dresnok walisema kuwa alikuwa mtiifu kwa Korea Kaskazini hadi mwisho, kwenye mahojiano ya video iliyochapishwa wiki iliyopita.
Baada ya kuvuka na kuingia Korea Kaskazini mwaka 1962, alianza kuishi maisha yasiyo ya kawaida mjini Pyongyang.
Hi ni pamoja na kuibuka kwa nyota wa filamu katika sekta ya filamu nchini Korea Kaskazini.
Uvumi kuhusu kifo cha bwana iliibuka mapema mwaka huu, na video ya hivi punde ya wanawe Ted na James Jr wakiwa wamevaa sare za jeshi na wakizungumza kwa ufasaha lugha ya kikorea
![Screenshot of North Korean television interview with James Dresnok's sons](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/12C11/production/_97471867_52ab5fa4-bf0e-4116-9895-f37547332a01.jpg)
"Kitu kimoja ambacho baba yetu alituomba tufanye ni tuwe wafanyakazi watiifu, kujitolea kwa kiongozi Kim Jong-Un na kuwalea watoto wetu waweze kufuata mwelekeo sawa na huo".
Video hiyo ilichapishwa na mtandao na shirika la habari la Korea Kaskazini la Uriminzokkiri wiki iliyopita.
Hii ni mara ya pili wanaume hao wawili wameonekana kwenye shirika hilo. Mwaka 2016 walionekana wakiisifu Korea Kaskazini kwenye kanda nyingine ya video.
Wote walisema kuwa wako kwenye jeshi la Korea Kaskanizini, wameoa na wana watoto.
Leave a Comment