SARATANI YA TITI YAMPA UMAARUFU INSTAGRAM.
Wakati alipokuwa akiugua saratani ya titi, Alison Habbal alikuwa akihisi kuchoka.
Akiwa miaka 36 wakati alipoanza kuugua ugonjwa huo, Alison ambaye ni raia wa Sydney alijua kwamba atapoteza nywele zake na titi lake hatahivyo mpango wa kutengeza titi jingine kupitia upasuaji wa kutumia plastiki haukumvutia.
Wakati wote alipokuwa mgonjwa aliwatafuta wachoraji tatoo katika mitandao, na baada ya majadiliano marefu Alison akaamua kumpa kazi ya uchoraji huo msanii kutoka New Zealand, Makkala Rose, mwenye umri wa mika 23.
Tatoo hiyo ilichorwa mjini Melbourne kwa saa 13 mnamo tarehe mosi mwezi Julai.
Alison alifurahia kazi hiyo na akaamua kuchapisha picha yake katika mitandao ya Instagram na facebook na kumpatia umaarufu mkubwa miongoni mwa wateja wa mitandao hiyo.Wengi walisifu wazo lake.


Leave a Comment