KUPATWA KWA JUA KUMETOKEA TENA, HIVI NDIVYO UKWELI HALISI.

KUPATWA KWA JUA.
Hatimaye leo tumeshuhudia tena kupatwa kwa jua, hali halisi inavyokea nikama ifuatavyo;
Hali hii inatokea kama dunia, mwezi na jua zinakaa kwenye mstari mmoja mnyoofu yaani wakati mwezi unapita kati ya dunia na jua.
Katika hali hiyo kuna kivuli cha mwezi kwenye uso wa dunia,kivuli hiki hakifuniki dunia yote. Kwa hiyo kupatwa kwa jua kunaonekana kwa watu wengi kama kupungua kwa mwanga wa jua.
Nikila baada ya miaka mitano hali hii huwa inatokea katika mzunguko wa sayari ambapo leo pia tarehe 1/9/2016 tumeshudia mwezi ukipita katikati ya jua na dunia.
                                        AINA ZA KUPATWA KWA JUA..
kupatwa kabisa:
jua lapotea kabisa kwa dakika chache. Hali hii yaonekana kwenye kanda nyembamba duniani kinapopita kitovu cha kivuli.
kupatwa kipete:
mwezi huonekana mdogo kuloko jua. Kwa hiyo duara ya kung'aa ya jua ni kubwa kuliko duara ya mwezi na mwanga wa jua waonekana kama pete.
kupatwa kwa jua kisehemu:
Katika eneo kubwa la kivuli cha kando watu hona upungufu wa mwanga; kiasi chake hutegemea umbali na kitovu cha kivuli. Wakitazama jua kwa filta kwa mfano kioo kilichopakwa dohani katika moshi ya mshumaa huwa wanaona sehemu ya duara ya jua imefunikwa.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.