MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI WILAYANI KIBITI.
Mkazi mmoja wa kitongoji cha Nyambwanda kilichopo katika Kijiji cha Hanga wilayani Kibiti aliyetambulika kwa jina la Hamis Ndikanye (54) ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumamosi akiwa nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa marehemu alijitambulisha kwa jina la Hamis Saidi amesema watu kama watano wakiwa na bunduki walifika nyumbani kwa ndugu yake saa 6 usiku, kisha kufanya mauaji hayo.
Alisema kabla ya kufanya mauaji hayo walimfunga mke wa marehemu kitambaa usoni na kisha kumpiga risasi mbili mume wake.
Mganga wa Kituo cha Afya Kibiti Dk Sadock Bandiko amesema Ndikaye alipigwa risasi mbili mwilini mwake, moja kichwani na nyingine mgongoni.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Rufiji, Onesmo Lyanga, amesema polisi wako eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi.
Leave a Comment