ALIYEKUWA MWANAJESHI WA UINGEREZA AUAWA KENYA
Tristan Voorspuy aliuawa na wafugaji wakati alipoenda kuchunguza baadhi ya nyumba zake ambazo zilikuwa zimechomwa na washambuliaji hao.
Laikipia na kaunti jirani zimekuwa zikikabiliwa na viwango vya juu vya ghasia zinazosababishwa na wafugaji ambao wanatafuta lishe ya mifugo yao lakini, wachanganuzi wanasema kuwa utovu huo wa usalama umesababishwa na siasa.
Wamiliki wa mashamba makubwa mjini Laikipia wameitaka serikali kueka usalama katika eneo hilo.
Wanahofia kwamba tatizo hilo huenda likaenea katika kipindi cha wiki zijazo huku ardhi ya lishe ikipungua katika maeneo ya wafugaji hao kutokana na ukame katika maeneo ya kaskazini mwa taifa hilo.
Wakati huohuo kuna hali ya wasiwasi katika kaunti jirani ya Baringo baada ya serikali kupeleka mamia wa maafisa wa usalama na kutoa agizo la kupiga risasi wafugaji wanaofanya mashambulio.
Leave a Comment