KAMATI YA SAA 72 YAIPA SIMBA POINTI TATU.
Simba ilikata rufaa ikitaka ipewe pointi tatu kwa kuwa Kagera Sugar ilimchezesha Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano.
Katika mechi hiyo, Simba ililala kwa mabao 2-1 na baada ya hapo, ikatangaza kutangaza kukata rufaa.
Katika kikao cha jana, Simba imeshinda rufaa hiyo baada ya kubainika kuwa Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano.
Kutokana na Simba SC kupewa pointi tatu sasa itafikisha jumla ya pointi 61 na kuwa kinara wa ligi kuu, ikifuatiwa na Yanga SC yenye pointi 56 na michezo miwili mkononi.

Leave a Comment