RAIS MAGUFULI KUPOKEA TAARIFA YA VYETI FEKI LEO.


RAIS John Magufuli leo anatarajiwa kupokea taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma katika Ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.

Taarifa iliyotolewa jana na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais katika Ikulu Ndogo ya Chamwino Dodoma, Jaffar Haniu ilisema taarifa hiyo itawasilishwa kwa Rais Magufuli na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki.

Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma liliendeshwa na Serikali kuanzia Oktoba, 2016.

Hivi karibuni wakati akifungua rasmi nyumba mpya za makazi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Rais Magufuli alisema anasubiri ripoti kuhusu watumishi wa umma wenye vyeti feki wapatao 9000.

“…Kwa hiyo mnaweza mkaona shida zilizopo katika nchi hii, huku wafanyakazi hewa karibu 19,000, wanafunzi hewa ni zaidi ya 56,000, kila mahali unapokwenda ni matatizo, lakini ni lazima niyatatue matatizo kwa sababu mlinichagua kwa ajili hiyo,”
alisisitiza Rais katika hotuba yake hiyo.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.