Serikali yagharamia msiba wa wa Wanafunzi Waliofariki Arusha


Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania imegharamia Sanda pamoja na majeneza kwa ajili ya Wanafunzi wa Shule ya msingi Lucky Vicent waliopoteza maisha mapema jana kwenye ajali iliyokuwa ikihusisha safari ya kimasomo.

Akitoa taarifa hiyo leo Meya wa Jiji la Arusha , Mh. Calist Lazaro amesema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa tayari Serikali imekwishalipia gharama za majeneza na sanda ya kuhifadhia miili ya marehemu ambao kesho wanatarajiwa kufanyiwa ibada katika Uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.