TANZIA : MMILIKI WA HOTELI ZA NGURDOTO, NAURA SPRING, IMPALA ZA ARUSHA AMEFARIKI DUNIA
| Mmiliki wa Hotel hizo ndugu Mrema amefariki Dunia jana jumapili julai 30 2017 South Africa alipokwenda kwa Matibabu. |
Mfanyabiashara maarufu nchini, Maleu Mrema amefariki dunia jana akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.
Akizungumza na Mwananchi ndugu wa marehemu,Vincent Laswai alithibitisha msiba huo akiwa nyumbani kwa marehemu eneo la Uzunguni jijini Arusha.
Laswai amesema kwamba alipokea taarifa za kifo cha marehemu jana saa 12 jioni na uongozi wa familia utatoa taarifa za kifo cha mfanyabiashara huyo leo.
amesema kwamba ni mapema kuzungumzia chanzo cha kifo kwa sababu bado hawajapata taarifa kutoka katika hospitali aliyokuwa akitibiwa nchini humo.
Hivi karibuni marehemu Mrema alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya ambapo Juni mwaka huu alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.

Marehemu Bwana Faustine Meleo Auye Mrema ni mzaliwa wa Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.
The Impala Group of Hotels inajumuisha:
1) Impala hotel (Arusha)
2) Impala hotel (Moshi)
3) Ngurdoto Mountain Lodge (Arusha)
4) Naura Springs Hotel (Arusha)
5) Impala shuttle Services (Arusha)
6) The Classic Tours & Travels
Impala Hotel ambayo ndio hotel yake ya kwanza ilianzishwa mwaka 1988.
CHANZO:JAMII FORUMS
Leave a Comment