REAL MADRID YAILAZA BARCELONA.


Kwa mara nyengine Real Madrid imeilaza Barcelona 2-0 katika uwanja wa nyumbani wa Bernabeu na kuibuka mshindi kwa jumla ya mabao 5-1 na hivyobasi kushinda kombe la Super Cup.


Mabingwa hao wa Uhispania na Ulaya walitawala mechi hiyo licha ya kutoshoriki kwa nyota wao Cristiano Madrid.


Photo published for Real Madrid – FC Barcelona: Se escapa la Supercopa de España (2-0) | FC Barcelona

Marco Asensio ambaye pia alifunga katika ushindi wa mechi ya kwanza huko Barcelona aliwapatia mabingwa hao uongozi wa mapema kupitia mkwaju wa maguu 25.


Karim Benzema aligusa kwa uhodari pasi nzuri iliopigwa na Marcelo na kumwezesha kufunga bao la pili huku ikiwa wazi kwamba Barcelona wasingeweza kusawazisha.


Real Madrid ilicheza mechi hiyo kwa urahisi mkubwa huku Barca wakifanya mashambulio kupitia Lionel Messi na Suarez yaliogonga mwamba wa goli.


Akiwa kocha wa timu hiyo kwa miaka miwili pekee Zinedine Zidane ameiongoza Real Madrid kushinda mataji mawili ya vilabu bingwa na taji la La liga la 2016-17.

Photo published for Zidane: “Dos títulos para empezar la temporada está muy bien” | Real Madrid CF

Na kufuatia ushindi huo ni wazi kwamba haitakuwa rahisi kwa timu nyengine kuwabwaga mabingwa hao msimu huu.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.