Polisi Wataja Chanzo cha nyumba ya Zitto Kabwe Kuwaka Moto.
Nyumba hiyo ipo mtaa wa Kibingo, mji mdogo wa Mwandiga katika wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.
Amesema joto hilo limesababisha mlipuko wa moto kwenye betri za sola na hivyo nyumba kushika moto na kuteketea yote.
Polisi wanamshikilia mlinzi wa nyumba hiyo, Norbert Joseph kwa mahojiano zaidi ili kubaini kama kuna uzembe wowote uliofanywa na kusababisha moto kuwaka.
Msaidizi wa Zitto anayeifahamika kwa jina la Nyembo Mustafa ametaja thamani ya hasara iliyosababishwa na moto huo kwamba ni Sh 45 milioni.

Leave a Comment