Marekani yailaumu Korea Kaskazini kwa kirusi cha WannaCry
![]() |
| Thomas Bossert ambuye ni msadizi wa Rais Donald Trump, aliyesama haya kupitia jarida la Wall Street Journal. |
Utawala nchini Marekani unasema kuwa Korea Kaskazini ilihusika moja kwa moja na kirusi cha wannaCry kilichoadhiri hospitali, biashara na mabenki kote duniani mapema mwaka huu.
Kirusi hicho kilidaiwa kuvamia zaidi ya kampuni 300,000 kwenye mataifa 150 na kusababisha hasara ya mabilioni ya dola.
![]() |
| Kompiuta zinazotumia Windows zilivamiwa na kirusi hicho na kufungwa ambapo watumiaji walitakiwa kulipa ili kuweza kupata data zao |
Bw. Bossert anayemshauri Trump katika masuala ya usalama wa ndani wa nchi alisema kuwa madai hayo ni kutokana na ushahidi uliopo.
Serikali ya Uingereza na kampuni ya kompiuta ya Microsof waliilaumu Korea Kaskazini kwa kirusi hicho.
Mwezi Mei kompiuta zinazotumia Windows zilivamiwa na kirusi hicho na kufungwa ambapo watumiaji walitakiwa kulipa ili kuweza kupata data zao.
![]() |
| Korea Kaskazini haijajibu madai hayo |



Leave a Comment