Kundi La GWT Kumuenzi Marehemu Fanuel Sedekia.
Baada Ya Kumaliza Mwaka 2017 Kwa Kishindo Kwa Kuachia Video Ya Wimbo Wao Mpya Unaokwenda Kwa Jina La “Ntemi” Tarehe 24 Dec 2017, Kundi Linalofanya Vizuri Hapa Nyumbani Tanzania Glorious Worship Team Sasa Wanaandaa tamasha Kubwa la Kuenzi Huduma Iliyofanywa Na Marehemu Fanuel Sedekia.
Kuthibitisha Taarifa Hii Kiongozi Wa Kundi Hilo Emmanueli Mabisa Aliandika Ujumbe Akisema;
“Ile Event Ambayo Inasubiliwa Kwa Hamu Sana Itakayofanywa Na Kundi Zima La GWT Ya Kumbukumbu Ya Kuenzi Huduma Kubwa Aliyoifanya Fanuel Sedekia ….Mwaka Huu Itafanyika Na Hakika Utabarikiwa Na Kukumbuka Kazi Kubwa Aliyoiacha Mtumishi Wa Mungu Sedekia… Pichani Nikiwa Na Aliyekuwa Mke Wa Marehemu Fanuel Sedekia ARUSHA…..”
Event Hiyo Inatarajiwa Kufanyika Dar Es Salaam Kwanza Na Baadae Arusha.
Endelea Kufatilia HABARI ZONE Tutakuletea Tarehe Na Mahali Ambapo tamasha hili litafanyika.
Leave a Comment