MWIMBAJI ATOSHA KISSAVA ASHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA
Mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za injili, mwanadada Atosha Kissava anayetamba zaidi na wimbo wake unaoitwa "KILA MTU ANASEMA UMWEMA" alioutoa mwaka jana hii leo januari 6 anasheherekea siku yake ya kuzaliwa
Siku ya kuzaliwa ni siku muhimu sana kwa kila binadamu hapa chini ya jua, kupitia ukurasa wake wa facebook Atosha amemshukuru mwenyezi Mungu kumpa tena mwaka mwingine wa kumtumikia zaidi.
"HAPPY BIRTHDAY TO ME!Karibu rafiki Uungane na mimi kumshukuru Mungu kwa kunipa Mwaka mwingine wa Kuendelea kumtumikia...GLORY TO GOD!🙌#2018 MY YEAR OF NEW DAWN ERA
#MY CASE IS DIFFERENT" Aliandika Atosha Kissava
#MY CASE IS DIFFERENT" Aliandika Atosha Kissava
Mbali na fanikio katika huduma yake ya uimbaji, Kwa mwaka 2017 kwa upande wake ulikuwa ni mwaka wa mafanikio makubwa kwake, aliweza kufanikisha kupata mchumba aliyefunga naye ndoa desemba 2017.
Pia mwaka 2017 kuna mambo mengi aliyojifunza "Yako mengi Nimejifunza kama ATOSHA mwaka 2017, baadhi ni;1.SIO VITA ZOTE UNAWEZA KUZISHINDA KWA KUPIGANA,VITA NYINGINE UNAZISHINDA KWA KUKAA KIMYA tu. Unatunza amani yako NA KUSONGA MBELE kwa speed ya 4G💪 💪💪 Jambo lingine jingine nililojifunza 2017 ni 2. SIO KILA BAYA LINALOKUPATA LIMELENGA KUKUANGAMIZA,NO! MABAYA MENGINE YANARUHUSIWA YATUPATE KTK MAISHA ILI KUTUIMARISHA,kuna mambo mengi sana yalikuja kama mabaya ktk maisha yetu lakin Mwisho wake umekuwa, mwema sana kwa hayo Tumekuwa ushuhuda kwa wengi. Sijui wewe umejifunza nini kwa mwaka mzima huu 2017?" aliandika katika ukurasa wake wa faceboook
Leave a Comment