VUMILIA NG'UNDA AACHIA 'KOMBORA' JIPYA


Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Vumilia Ng'unda anayefanya vizuri na albamu yake ya "VUTA SUBIRA" ambayo anaisambaza hivi sasa, ameachiliwa wimbo mpya kwa mwaka 2018.

Akifanya mahojiano na HABARI ZONE MEDIA chini ya mkurugenzi Jackson Fanuely, mwimbaji huyo amesema wimbo wake mpya unaoitwa "TUMECHAGULIWA" ni mahususi kwa shukrani kwa mwenyezi MUNGU kwani ametuchagua kuuona mwaka 2018 hivyo tuzidi kumuabudu na kumtukuza

"nimeamua kuachia wimbo huu kwa sababu Mungu anapo kuchagua kuuona mwaka 2018 au kuzidi kuwepo ni kwamba anao mpango na wewe, amekupa pumzi na afya hivyo mwaka huu tuzidi kumtumikia zaidi zaidi kwa nguvu zote" amesema mwimbaji Vumilia Ng'unda.

Kwa mujibu wa muimbaji huyo wimbo huu mpya("TUMECHAGULIWA") haupo katika albamu yake anayoisambaza hivi sasa inayoitwa "VUTA SUBIRA" bali ni wimbo ambao unaojitegemea ikiwa ni maandalizi ya albamu impya.

Kusu video ya albamu yake na wimbo huo amesema yupo kwenye mchakato wa kuaanda video kali na nzuri ya kimataifa.

Vumilia Ng'unda ni moja ya waimbaji wa kubwa kutoka Kilimanjaro ambaye pia ni mwalimu wa muziki mbali na uimbaji.

Kwa mawasiliano unaweza kumpata kwa Namba za Simu 0753 885 935.


TAZAMA VIDEO VUMILIA NG'UNDA AKIFANYA MAHOJIANO


Pia kama wewe ni muimbaji unahitaji kufanya Interview na HABARI ZONE MEDIA karibu sana tuwasiliane kwa namba 0768 102 984 AU 0689454357. Asante

Usiache Kufatilia HABARI ZONE media kila siku kuhusu story za wasanii na habari mbali mbali za kijamii, tunapatika Facebook, Twitter, Whatsapp Goup(0768102984) na Instgram.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.