Yaliyojiri wakati Msemaji Mkuu Wa Serikali Alivyokuwa na mkutano na Waandishi WA Habari Leo Machi 5
*YALIYOJIRI WAKATI WA MKUTANO WA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI DKT. HASSAN ABBAS NA WAANDISHI WA HABARI LEO TAREHE 5 MACHI, 2018 MJINI DODOMA*
#Mkutano huu ni mwendelezo wa mikutano ya kila mwezi kati ya Msemaji Mkuu wa Serikali na wanahabari kwa lengo la kutoa mrejesho kwa umma, kupitia wanahabari kuhusu kinachoendelea katika utekelezaji wa ahadi za Serikali.
# Hivi karibuni nilifanya ziara katika vyombo vya habari vya hapa Dodoma kwa lengo la kuona utendaji kazi na kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
# Nawaomba Wanahabari, tuendelee kufanya kazi zetu kwa weledi mkubwa bila kukiuka misingi ya Taaluma.
# Nawakumbusha wale wote ambao hawana "Press Card", hapa Dodoma zipo wakamilishe taratibu kuanzia April mosi itakuwa mwisho.
# Nitoe wito kwa wanahabari wa Dodoma kufuata maadili na Misingi ya uandishi wa habari.
# Kufikia Februari 2018, Serikali imeendelea kutekeleza ahadi zake mbalimbali kwa wananchi kwa lengo la kufikia maisha bora kwa kila Mtanzania.
# Kwa mwezi huu tumeonya magazeti matatu yanayoenda kinyume na maadili ya uandishi.
# Katika mwezi huu tutaangalia mambo makubwa sita(6) yafuatayo:
1.Tanzania Kimataifa
2. Madeni ya watoa huduma, watumishi
3. Uzalishaji wa Umeme Kinyerezi na Stiglers
4. Ununuzi wa Treni mpya
5. Ahadi ya Meli mpya Maziwa Makuu
6. Ujenzi wa Viwanja vya ndege nchini.
*Tanzania Kimataifa*
# Serikali ya Tanzania imeendelea kung'ara kimataifa ambapo Ripoti ya Taasisi ya Kimataifa ya Transparency International iitwayo Curruption Perception Index 2017 imeonesha nchi yetu imepanda kwenda nafasi ya juu zaidi katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi kutoka ya 216 mwaka 2016 hadi 203 mwaka 2017
# Sisi kama Serikali tutaendelewa na jitihada mbalimbali kuhakikisha tunapambana na rushwa nchini.
# Katika nchi za Afrika Mashariki, Tanzania imekuwa ya pili katika mapambano dhidi ya Rushwa na Ufisadi Nchini.
*Madeni ya watoa huduma, watumishi*
# Katika mwaka wa fedha 2017/2018 Hazina ilitenga kiasi cha Tzs Trilioni 1 kulipa madeni mbalimbali ya watoa huduma, wazabuni na watumishi wa umma.
# Mpaka Februari mwaka huu jumla ya Tzs Bilion 896.3 zimeshalipwa
*Uzalishaji wa Umeme Kinyerezi na Stiglers Gorge*
# Serikali pamoja na miradi mingine mbalimbali nchini inatekeleza miradi miwili mikubwa ya uzalishaji wa umeme wa gesi ambayo ni Kinyerezi I Extension( Megawati 185) na Kinyerezi II wa megawati 240.
#Mradi wa Kinyerezi II ambao utazalisha Megawati 240 unatekelezwa kwa asilimia 15 fedha za Serikali( ambazo zimeshatolewa) na asilimia 85 ni mkopo.
# Mpaka sasa Mradi umefikia asilimia 90 kukamilika ambapo kufikia Februari 2018 jumla ya megawati 111.88 zimeshaingizwa katika gridi ya Taifa.
#Mradi wa kihistoria wa Stiglers ukikamilika utazalisha jumla ya Megawati 2100 ambazo ni zaidi ya mara mbili ya umeme unaotumika kwa sasa nchi nzima.
*Ununuzi wa Treni mpya*
# Katika taarifa ya Januari, 2018 tulieleza ununuzi wa mabehewa ya kisasa ya abiria na ya mizigo takribani 1,590 vichwa takribani 25 na mitambo mengine.
#Takribani Kampuni 54 zimejitokeza ambapo kati ya hizo 35 zimerejesha nyaraka za zabuni kutoka mataifa mbalimbali na tathimini inaendelea
*Ahadi ya Meli mpya Maziwa Makuu*
# Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi kuwaondolea adha ya usafiri wananchi wa Maziwa Makuu ya nchi yetu likiwemo Ziwa Nyasa, Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria.
#Meli mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1200 na mizigo tani 400 Ziwa Victoria, mkandarasi amepatikana na majadiliano ya mwisho na kusaini Mkataba na Kampuni ya STX ya Jamhuri ya Korea vitafanyika mwaka huu.
# Katika Ziwa Tanganyika, Zabuni kwa ajili ya utengenezaji wa Meli mpya ya abiria na mizigo itatangazwa mwezi huu.
#Meli ya kisasa katika Ziwa Tanganyika itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo na italeta mapinduzi makubwa katika usafiri ziwani humo.
*Ujenzi wa Viwanja vya ndege nchini.*
#Julai mwaka huu nchi yetu itapokea ndege kadhaa mpya ikiwemo *Boeing Dreamliner* hivyo ukarabati wa viwanja vya ndege vya Kitaifa, Kimataifa na Kimkoa unaendelea kwa kasi nchini.
# Ujenzi wa Terminal III Dar es Salaam uko zaidi ya asilimia 50, Jengo la Abiria Uwanja wa Kimataifa wa Songwe lipo asilimia 57.
# Viwanja vingine zaidi ya 10 ujenzi au ukarabati unandelea kuanzia Kigoma, Tabora,Mwanza Geita, Shinyanga, Sumbawanga, Mtwara, Musoma n.k.
*Imeandaliwa na Idara ya Habari- MAELEZO*

Leave a Comment