TP MAZEMBE KUSAJILI MCHEZAJI WA YANGA.
Moja ya kauli zilizotolewa na TP Mazembe walivyotua Tanzania kucheza na YANGA wamepanga kuondoka na wachezaji wenye vipaji kutoka Tanzania kama walivyofanya kwa Mbwana Samatta.
Baada ya mechi hiyo ya juzi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam na kuibuka na ushindi wa bao 1-0, jina la winga mpyawa Yanga, Juma Mahadhi, ndio lilinasa kwenye akili za mashabiki na mabosi wa Mazembe kama ilivyokuwa kwa Samatta mwaka 2011.
Mahadhi ambaye alikua anacheza mechi yake ya kwanza akiwa na jezi ya Yanga, umewashawishi mashabiki na viongozi wa mazembe kubeba jina la kinda huyo na kupania kulipeleka kwa tajiri wa klabu hiyo, Moise Katumbi.
Inafahamika kuwa Katumbi anawakubali na kuwaamini sana sana mashabiki wake na siku zote wakimpa jina la mchezaji huwa tayari kuvunja benki kumsajili kama alivyofanya kwa Samatta miaka mitano iliyopita.
Mahadhi alionyesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo.
Leave a Comment