VIDEO: Fahamu Mti Unao Wasaidia Watu Kupata Wapenzi

Mwaloni wa Bwana Harusi (Bridegroom's Oak

Huko Ujerumani kuna mti mkubwa aina ya Mwaloni (Kwa Kiingereza huitwa Oak Tree), Kwenye mti huu kuna tobo watu waliopo single yaani wasio na wapenzi huweka barua zao za kutafuta wapenzi.
Mtu yeyote anaweza kuchukua barua na kuijibu, Kwa mwaka takribani barua elfu moja (1,000) huwekwa hapo, Takribani ndoa mia moja (100) hufungwa kupitia mti. Mti huu pia ulikuja kuitwa Mwaloni wa Bwana Harusi (Bridegroom's Oak).
Miaka 130 iliyopita,  Kijana mmoja aliyekuwa akijihushisha na biashara ya kutengeneza na kuuza Chocolate huko Ujerumani. Kijana huyo anaitwa Wilhelm. Siku moja alikutana na msichana mrembo sana, binti wa mlinzi wa misitu ya Dodau Forst huko Ujerumani.Mrembo huyo alikuwa akiitwa Minna. Kijana Wilhelm alimpenda sana binti huyo, alifanikiwa kuwa na kwenye mahusiano na mrembo Minna. Baada ya muda Baba yake na Minna alijua wazi mahusino ya binti yake, hakukubali uhusiano wa mwanaye na kijana huyo, Wapenzi hao wawili walivunjika moyo.
Wapenzi hao Waliamua kwamba wanapaswa kutafuta njia ya kuendelea kuwasiliana. Kisha walipata mti mzuri aina ya OAK kwa kiswahil mti wa Mwaloni, ulikuwa mbali kidogo na nyumbani kwa kina Minna. 
Walikuwa wakiachiana barua za mapenzi kwenye tobo la mti huo. Waliendelea kutuma barua kwa kila mmoja kwa muda, lakini siku moja baba wa msichana alikujapogundua na kisha aliwapa idhini ya kuoana.  Nadhani aligundua kuwa asingeweza kuzuia upendo wa kweli uliojengeka kati yao. Wote hawakupoteza muda, Wilhelm akamuoa Minna, Walifunga ndoa Juni 2/1891. Tena harusi yao ilifanyika chini ya mti wao wa siri wa mwaloni.


Hadithi hii moja ndogo ya mapenzi ilisababisha na kuleta matokeo ya watu wengine wengi kuipenda kwa miaka iliyofatia,  Wakati hadithi hii ilipozidi kusambaa na kujulikana kila kona, kwa mara ya kwanza mti wa mwaloni uliitwa “The Bridegroom’s Oak” kwa kiswahili" Mwaloni wa Bwana Arusi ".
Tangu wakati huo, watafutaji wa mapenzi wamekuwa wakiweka barua zao kwenye mti huo, kwa matumaini ya mtu kuipata na kuijibu.  Mnamo 1927, mti ulianza kupokea barua nyingi sana, Na kisha mti huo ulipata anwani yake na kuliwekwa mfanyakazi wa posta.

Karl-Heinz Martens, ambaye ni mfanyakazi wa posta aliyepewa kazi katika mti huo wa Mwaloni wa Bwana harusi, alifanya kazi hapo kwa miaka 20. Lakini hadithi ya mapenzi ambayo inapendwa zaidi kutoka katika mti huo, ni ya Martens mwenyewe! Mnamo 1989, kituo kimoja cha Runinga kilikuja kutoa habari katika mti huo, walifanya mahojiano na mfanyakazi huyo wa posta Bw. Martens.  Walimuuliza swali Martens ikiwa amewahi kupata mpenzi kwa msaada wa mti huo, na akasema kwamba hakuwahi kupata.  Siku chache tu baada ya kipindi hicho cha Televisheni hiyo kurushwa hewani, Martins aliona barua iliyoandikwa kwa mkono iliyoelekezwa kwa kwake. Barua hiyo ilitoka kwa mwanamke aliyeitwa Renate ambaye inaonekana alitaka kukutana naye.  Hakika ni historia kubwa, huwezi amini, Wawili hao walioana, na walipiga picha zao chini ya Mti huo uliowakutanisha ,Picha hizo zilichapishwa katika habari kwenye magazeti huko Ujerumani.  Wanandoa hao hata hivyo, walishinda tuzo ya Harusi bora ya Mwaka. Wawili hao bado wanaishi kwa furaha hadi leo. 

Kwa hivyo, ikiwa wewe au mtu unayemjua anatafuta mapenzi au rafiki wa kuandikiana barua, unaweza kutuma barua kwa Mwaloni wa Bwana Arusi! Anwani ni: Bräutigamseiche, Dodauer Forst, 23701, Eutin, Ujerumani.

Anwani ya Mwaloni Wa Bwanaharusi ni: 
Bräutigamseiche, Dodauer Forst, 23701, Eutin, Ujerumani.

FUNGUA VIDEO KUTAZAMA ZAIDI KUHUSU MWALONI HUU

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.