HIVI NDIVYO UBONGO WA MWANAMKE UNAVYOFANYA KAZI KWA HARAKA ZAIDI KULIKO WA MWANAUME.


Ubongo wa mwanamke ni mdogo kwa 8% kuliko wa mwanaume, lakini unamuungano wa mawasiliano (interconnections) nzuri sana kuliko wa mwanaume, na ndio mana mwanamke anaweza kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja bila kukosea (multi-tasking).

Itakua umeshaona kwa wakati huohuo mwanamke anapika, anaangalia tamthilia kwenye TV, anasuka nywele n.k. na vyote hufanya kwa ufanisi, lakini mwanaume amalize kimoja kwanza ndio ahamie kingine.

Ubongo wa mwanamke unauwezo wa kufanya mawasiliano ya haraka sana (fast data transfer) kuliko wa mwanaume, hivyo mwanamke anao uwezo mkubwa wa kuwasiliana, kusoma lugha za maumbile, kufikiri na kutabiri yajayo (situational thinking) kwa urahisi na haraka zaidi, yani mara 10 zaidi ya mwanaume. Ndio mana, mwanamke anauwezo wa kujenga mahusiano ya kijami kirahisi (social thinking and interaction) zaidi ya mwanaume.

Umeshawahi gundua upo na mwanamke labda mpo beach au kwenye gari, alafu ukataka kumbusu (kiss) kwa kumstukiza Sasa kile kitendo cha wewe kuwaza kumbusu, utakuta yeye alishagundua dakika chache zilizopita kabla yako, kupitia mihemko ya mwili wako. 

Na kama hayupo tayari, anao uwezo wa kukwepesha mdomo wake haraka zaidi kabla ya wewe kumfikia, bila kujali alikua ktk mazingira gani au akifanya nini.

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.