ROSE MUHANDO KUTOA ALBAMU MPYA BAADA YA KIMYA KIREFU

Rose Muhando

Baada Ya Kimya Cha Muda Mrefu Katika Tasnia Ya Muziki Wa Injili, Sasa Muimbaji Wa Nyimbo Za Injili Tanzania Rose Muhando ameamua Kurudi Rasmi Huku Ikitangazwa Ujio Wa Album Yake Mpya.

Album Yake Mpya Itatambulishwa April 1 mwaka huu Siku Ya Tamasha La Pasaka Jijini Mwanza Na April 2 mkoani Simiyu.

Hayo Yamethibitishwa Na Muandaaji Wa Tamasha La Pasaka Linalofanyika Mara Moja Kwa Mwaka Alex Msama.

Katika Maelezo Yake Alex Msama Amesema “Tunakuja Na Waimbaji Wengi Huko, Waimbaji Wa Kimataifa, Waimbaji Wakubwa Wengi. Na Katika Tamasha Lile La Pasaka Yako Matukio Mengi Makubwa Ya Pasaka Yatafanyika Lakini Lipo Tukio Moja Ambalo Hili Nalitaja, Tukio Hilo Ni Uzinduzi Wa Album Ya Rose Muhando. Amekuwa Kimya Kwa Muda Mwingi Sana Lakini Kipindi Hichi Anakuja Sasa Na Anaibuka Na Album Yake Mpya Ambayo Ataizindua Rasmi Katika Uwanja Ule Wa Ccm Kirumba Tarehe 1/4 Pale Mkoani Mwanza. Tukitoka Mwanza Pia Tutakwenda Kuzindua Simiyu.”

No comments

TUFATILIE TWITTER

Powered by Blogger.