Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Dkt. Amani Walid Kabourou amefariki dunia
Mbunge wa zamani wa Kigoma Mjini, Dk Aman Kabourou amefariki dunia jana Machi 6, 2018 saa tano usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akitibiwa.
Msemaji wa Muhimbili, Neema Mwangomo amethibitisha kifo cha mwanasiasa huyo na kubainisha kuwa alifikishwa hospitalini hapo akitokea mkoani Kigoma.
“Amefariki dunia Machi 06, 2018 saa 5 usiku alifikishwa Muhimbili Machi 4, 2018 akitokea Hospitali ya Mkoa wa Kigoma. Alifikishwa Muhimbili akitokea Kigoma saa saba mchana,” alisema Mwangomo.
Dk Kabourou amewahi kuwa mbunge wa Kigoma Mjini mwaka 1995 hadi 1999 na 2000 hadi 2005 kwa tiketi ya Chadema. Mwaka 2006 alijiunga CCM na kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
Pia amewahi kuwa mwenyekiti wa chama tawala mkoani Kigoma kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2017.
Leave a Comment