VIDEO: IFAHAMU DINI INAYO MUABUDU DIEGO MARADONA / IGLESIA MARADONIANA
Kanisa la Maradona |
Kanisa la Maradona Ni dini iliyoundwa na mashabiki wa mwanasoka mstaafu wa Argentina Diego Armando Maradona, ambaye wanaamini kuwa mchezaji ni bora wa wakati wote.
Kanisa hilo linamuabudu Diego Maradona kama mungu |
Lakini Maradona yeye ni Mkatoliki na anamuheshimu mwenyez Mungu, katika sehemu kubwa ya kazi yake ya mpira wa miguu. Aliwahi kusema:
Mungu ananifanya nicheze vizuri. Ndio sababu kila wakati mimi
hufanya ishara ya msalaba ninakwenda uwanjani. Ninahisi ningekuwa
nikimsaliti ikiwa singefanya hivyo’’ alisema Maradona.
Nukuu za Maradona zenye utata
zinazohusiana na goli alilofunga wakati Argentina ilipokuwa ikicheza dhidi ya
Uingereza kwenye Kombe la Dunia la 1986, zinahisiwa kuwa zilipelekea mashabiki
wake kuhisi Maradona ni mungu na kuanzisha kanisa hilo linalomuabudu.
Maradona alifunga bao kupitia mkono wake, na mwamuzi wa mechi hiyo hakuona na kisha kuhesabu kuwa ni goli halali.
Baada ya kufunga bao hilo
Maradona alisema kwa vyombo vya habari "Nilifunga bao kidogo kwa kichwa na kidogo kwa mkono wa Mungu."
Hivyo basi goli hilo liitwa MKONO WA MUNGU.
Kanisa la Maradona lilianzishwa mnamo Oktoba 30, 1998 (siku ya maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa kwa Maradona) katika mji wa Rosario , Argentina na Mashabiki watatu ambao ni Héctor Campomar, Alejandro Verón na Hernán Amez.
Héctor Campomar, Alejandro Verón na Hernán Amez |
Alejandro Verón, ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa dini ya maradoniana alinukuliwa mwanzoni mwa uanzilishi wa kanisa hilo akisema " Nina dini ya busara, na hiyo ni Kanisa Katoliki , na nina dini iliyopitishwa juu ya moyo wangu, shauku yangu, na huyo ni Diego Maradona." Alisema Bw. Veron.
Wafuasi wa Kanisa la Maradonia ambao wapo zaidi ya nusu milioni kutoka sehemu mbalimbali ulimwengu kama vile Bolivia, Colombia, Brazil, Uruguay, Ufaransa na Canada, wamekuwa wakihesabu miaka hadi sasa, tangu kuzaliwa kwa Maradona mnamo Oktoba 30 1960.
Tarehe na mwezi huo aliozaliwa Diego Maradona, waumini hao huadhimisha siku hiyo kama Chrismas kwao, yaani siku aliyozaliwa mesia wao na hufanya ibada ya kumkaribisha messia katikati yao.
Siku hiyo kanisa hupambwa kwa rangi nyeupe na bluu ambayo ni rangi ya bendera ya taifa la Argentina na kubandikwa picha za Diego Maradona akiwa anatabasamu, ibada hiyo huitwa "Diego nuestro" kwa lugha ya Kihispania.
Amri Kumi za kanisa la Maradoniana |
Amri Kumi za kanisa la Maradoniana;
1. Kamwe usiuchafue mpira .
2.
Penda mpira wa miguu
kuliko vyote vingine.
3.
Tangaza upendo usio na
masharti kwa Diego na uzuri wa mpira wa miguu.
4.
Tetea fulana ya
timu ya taifa ya Argentina.
5.
Eneza habari ya
miujiza ya Diego katika ulimwengu wote.
6.
Heshimu mahekalu
ambayo Diego alicheza na mashati yake matakatifu.
7.
Umsitangaze Diego kama
mshiriki wa timu yoyote.
8.
Hubiri na kueneza
kanuni za Kanisa la Maradona.
9.
Weka jina Diego kama
jina lako la katikati ya majina yako.
10. Mpe mwanao wa kwanza kiume jina Diego.
TAZAMA VIDEO KUFAHAMU DINI YA MARADONA ZAIDI
Leave a Comment